"Bam Bam" Ya D Voice Na Zuchu Yaandika Rekodi Nyingine Kwenye Muziki

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Kama unaipenda ngoma ya "Bam Bam" ya D Voice akiwa amemshirikisha msanii  Zuchu basi habari njema ni kuwa video ya ngoma hiyo imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube

Video ya "Bam Bam" iliingia sokoni mwezi Novemba mwaka 2023 ambapo ilikuwa ni video ya kwanza kwa D Voice tangu aingie WCB Wasafi ikiwa imeongozwa na Director Folex.

Kufikia sasa video ya wimbo huo tayari imefikisha views Milioni 11 tangu kuachiwa kwake na ikiwa ndio video ya D Voice iliyofanya vizuri zaidi tangu aanze muziki.

Tangu aingie WCB Wasafi, D Voice ameshaachia video 6 ambazo ni Bam Bam, Lolo, Umenifunza, Mtamu, Mpeni Taarifa pamoja na Turudiane ambayo alimshirikisha Lava Lava.

https://youtu.be/JI8TLR3RNnU?si=hyvpZ7tg-3EQ4J2I

 

Leave your comment