Joseph Kusaga Awapatanisha Baba Levo Na Harmonize

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya miezi mingi ya uhasama na kufunguliana kesi mahakamani, hatimaye wasanii wawili wakubwa kwenye Bongo Fleva, Baba Levo na Harmonize wamepatanishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga. 

Wiki chache nyuma, Baba Levo alimshtaki Harmonize kwa kumpiga na kumjeruhi baada ya wawili hao kupishana na hatimaye kupigana kwenye sehemu ya kamari.

Ugomvi huo uliteka vichwa vya habari nchini Tanzania ambapo Baba Levo ambaye anajulikana kwa ushabiki wake mkubwa wa msanii Diamond Platnumz aliapa kumpeleka na kupata haki yake kwenye vyombo vya sheria.

Hivi karibuni Joseph Kusaga, CEO wa Clouds Media Group aliwakutanisha pamoja Baba Levo na Harmonize na kuonesha kuwa kwa sasa hakuna tofauti baina ya wasanii hao.

"Asanteni sana kwa kunipa heshima ya kukaa na kuongea kama baba yenu. Mmeniheshimu na nawashukuru sana sana maisha yaendelee" alizungumza Joseph Kusaga kwenye video hiyo ambayo inawaonesha Baba Levo na Harmonize wakiwa pamoja.

Leave your comment