Diamond Platnumz Atia Neno Baada Ya "Enjoy" Kufikisha Views Milioni 70

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga

Msanii kutokea Tanzania, Diamond Platnumz hivi karibuni ametia neno mara baada ya "Enjoy" ngoma ambayo ameshirikishwa na Jux kufikisha views Milioni 70 kwenye mtandao wa YouTube

Video ya "Enjoy" iliachiwa mwezi Agosti mwaka 2023 ambapo kwa mwaka jana, video ya ngoma hiyo ilisimama kama video ya muziki iliyotazamwa zaidi YouTube kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Juma Jux alichapisha video inayoonesha kuwa ngoma hiyo Imefikisha views Milioni 70 ambapo Diamond Platnumz alijibu kwa kuandika:

"70 Milioni kwa miezi 7. God is good, that means ikitimiza miezi 10 itakuwa na 100M na mwaka itakuwa na 120M." a

Leave your comment