Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Kisa Tems Na Ayra Starr, Ray C Atoa Darasa Kwa Wasanii Wa Tanzania
3 April 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Msanii mkongwe kunako kiwanda cha Bongo Flava, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C hivi karibuni amewatumia Tems na Ayra Starr kwa ajili ya kutoa darasa kwa wasanii wa Bongo.
Ray C ambaye ngoma zake kama "Uko Wapi" "Na Wewe Milele" na "Unanimaliza" zilimfanya kuwa maarufu Afrika Mashariki ametoa ushauri huo hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ray C ambaye kwa sasa anaishia huko nchini Ufaransa alichapisha video ambayo inawaonesha wasanii wawili kutoka Nigeria Tems na Ayra Starr wakiwa wanaimba ngoma ya Commas pamoja, pamoja na kwamba ngoma hiyo ni ya Ayra Starr.
"Halafu mnajiuliza mbona kama game ya imestuck?Pendaneni wenyewe kwa wenyewe kwanza..Mioyo yenu ikiwa safı ndani mkapendana wenyewe kwa wenyewe kwanza Lazma Milango mikubwa zaidi itafunguka kama inavyozidi kuwafungukia hawa wenzetu....Sio mambo ya kuchekeana usoni mkipeana migongo mnan'gon'gana Waii" aliandika Ray C
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Diso Ziod
21 April
- Lesson
20 April
- Drop new song loyo
21 April




Leave your comment