Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Kusah Adokeza Ujio Wa Collabo Kati Yake Na Ruby
29 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Msanii nguli kunako kiwanda cha Bongo Fleva, Kusah hivi karibuni amedokeza kuwa huenda kuna collabo inakuja baina ya msanii Ruby.
Kusah na Ruby ukiachana na kwamba ni wasanii lakini pia ni wazazi wenza ambao wana mtoto mmoja japo kwa sasa wametengana.
Akizungumza kwenye mazungumzo ya hivi karibuni, Kusah amedokeza kuwa kuna kipindi Ruby alimtafuta ili waachie collabo yao waliyofanya pamoja na Kusah aliongeza kuwa pamoja na tofauti zao za hapo awali lakini yeye binafsi alikubali ujio wa collabo hiyo
"Alinicheki Ruby aliniomba kuna nyimbo tulifanya zamani, kwamba anataka kuitoa. Ilikuwa ni sawa tu, tuliongea kibiashara na tulielewana" alizungumza Kusah
Ikumbukwe kuwa Kusah na Ruby tayari wameshatoa ngoma nyingine za pamoja ikiwemo "Kelele" pamoja na "Dondosha"
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Diso Ziod
21 April
- Lesson
20 April
- Drop new song loyo
21 April




Leave your comment