Ngoma 5 Mpya Kutoka Nchini Tanzania

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Wapenzi wa muziki kutoka Bongo wameendelea kupata burudani ya muziki mzuri kutoka kwa wasanii wawapendao bila kujali aina ya muziki.

Kutoka kwa wasanii kama Stamina Shorwebwenzi, Songa na Tunda Man hizi hapa ni ngoma mpya kutoka Tanzania

 

Tunaitaka Nusu - Tunda Man

Tunda Man amezidi kuonesha upendo alionao kwa timu yake ya Simba na hii ni baada ya msanii huyo kuachia Tunaitaka Nusu ngoma kali ambayo ndani yake msanii anaisifia timu yake ya Simba

Mkeka - Songa

Gwiji wa Hip Hop kutoka Tanzania, Songa amerudi tena na "Mkeka" ngoma kali ya Hip Hop ambayo si tu kwamba utapenda namna ambavyo Songa amechana lakini pia utaburudika na beat kali lilioundwa kwa ufundi wa aina yake.

Msanii Bora Wa Hip Hop - Stamina Shorwebwenzi

Kwenye kibao hiki Stamina hakuona hatari kueleza namna ambavyo anafanya vizuri kwenye rap ya Bongo, ngoma hii ikiwa ni mkwaju wake wa kwanza kwa mwaka 2024.

 

Je'taime - Beka Flavour Ft DJ Inno  

Beka Flavour ni fundi wa kuandika mistari na ndio maana kwenye mkwaju wake huu mpya, ukiachana na kuimba kwa Kiswahili lakni pia amenogesha kwa lugha ya kifaransa na kama unapenda ngoma kali na za kubembeleza basi hupaswi kutosikiliza mkwaju huu. 

Wali Nazi - Top Band Reunion

TID na Q Chief wameendelea kuthibitisha kuwa mafahali wawili wanaweza wakakaa zizi na ngoma yao mpya ya Wali Nazi ni uthibitisho toshana ndio mana mashabiki wameipokea ngoma hii kwa ukubwa wa aina yake.

Leave your comment