"Mi Sio Type Ya Kuingia Twitter Kujibizana" - Young Lunya

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii kutokea lebo ya Rockstar Young Lunya hivi karibuni ameacha freestyle ya ngoma ya Way Back ya kwake Country Wizzy akiwa na Jay Moe.

"Way Back" ni ngoma ya Country Wizzy ambayo kwa sasa inafanya vizuri nchini Tanzania ikiwa ni ngoma ya kwanza ya Country Wizzy kwa mwaka huu wa 2024

Kwenye moja ya mistari ya freestyle hiyo, Lunya alikaririwa akisema "Mimi Sio Type Ya Kuingia Twitter Kujibizana" mstari ambao umesababisha minong'ono baina ya mashabiki.

Young Lunya anajulikana kwa kutokupendelea kutumia mtandao wa Twitter kwani miezi mingi nyuma alisema kuwa watumiaji wengi wa mtandao huo hawamkubali

 

Kwa mwaka 2024, Lunya bado hajatoa ngoma yoyote.

Leave your comment