Rayvanny Akutana Na Davido Na Iyanya Afrika Kusini

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Rayvanny ameendelea kujitengenezea jina kwenye kwenye uwanja wa kimataifa na hii ni baada ya msanii huyo kukutana ana kwa ana na wasanii kutokea nchini Nigeria, Davido na Iyanya

Rayvanny amekutana na Davido pamoja na Iyanya huko Afrika Kusini ambapo kwa sasa msanii huyo kutoka Tanzania yupo kwenye ziara ya kimuziki kwani hapo awali msanii huyo alikuwa Ufaransa, India na Uingereza.

Iyanya na Rayvanny wamekutana tena ikiwa ni wiki kadhaa tu walipofanya hivyo Uingereza ambako pia waliingia studio na kurekodi.

Ikumbukwe kuwa Iyanya tayari ameshafanya kazi na wasanii wawili kutoka Tanzania ambao ni Ali Kiba kwenye "Huku Remix" na Diamond kwenye "Bum Bum" na "Nakupenda"

Davido pia alishafanya kazi na Diamond, Joh Makini na Dayna Nyange.

Leave your comment