Grammy Yamtaja Rosa Ree Kwenye List Yao Mpya

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga

Muziki wa Rosa Ree ambaye ni moja ya marapa wanaofanya vizuri kwa sasa nchini Tanzania umeendelea kupenya kwenye sehemu mbalimbali duniani na hii ni baada ya msanii huyo kupenya kwenye orodha ya Recording Academy ambao ni waandaaji wa tuzo za Grammy.

Rosa Ree ametajwa kwenye orodha ya wasanii 10 wa kike wa miondoko ya Afro Hip Hop wanaofaa kutazamwa zaidi. 

Kwenye orodha hiyo kuna wasanii wengine wa Kike toka Afrika kama Sho Madjozi wa Afrika Kusini, Femi One wa Kenya, Barony - Ghana, Nadai Nakai - Zimbabwe, na kutoka Nigeria ni pamoja na Candy Bleakz, SGaWD, Lifesize Teddy, Deto Black Eno na Deela.

Andiko hilo linatoa ufafanuzi wa kina kumhusu Rosa Ree na muziki wake, tangu alipoanza mwaka 2016 na ngoma ya "One Time" na kuonesha safari yake kwa uchache mpaka kufikia 2024.

Ukimuweka kando Rosa Ree, wasanii wengine kutoka Tanzania ambao wameshawahi kuhusiana na Grammy ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye mwaka 2022 alitumbuiza kwenye Grammy Global Spin Show

Leave your comment