Chin Bees Azindua Lebo Yake, Atambulisha Msanii Mpya

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Waswahili wanasema kimya kingi huleta mshindo mkuu na bila shaka usemi huo umeonekana wazi kwa rapa Chin Bees ambaye hivi karibuni ametambulisha msanii wake wa kwanza kwenye lebo yake mpya.

Chin Bees ni msanii kutoka Tanzania ambaye aliteka mioyo ya wana Afrika Mashariki miaka kadhaa nyuma kupitia ngoma yake ya "Pepeta" ambayo ilimtambulisha vyema kwenye muziki.

Hivi karibuni msanii huyo ametangaza kuja na lebo yake mwenyewe ya kuitwa BGE ambapo pia amemtambulisha Mr Furge kama msanii wa kwanza kusainiwa kwenye lebo hiyo.

Chin Bees na Mr Furge tayari wameachia ngoma mpya ya kuitwa "Make Me Crazy" ambayo humo ndani wameimba kwa lugha ya kiingereza.

Ikumbukwe kuwa miaka kadhaa nyuma, Chin Bees alikuwa amesainiwa chini ya Wanene Entertainment ambapo baada ya muda kupita msanii huyo aliachana na lebo hiyo.

Leave your comment