Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Zuchu, Ayra Starr na Tayla Watajwa Kwenye Orodha Ya Vijana Wenye Ushawishi Afrika
27 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Msanii kutokea Tanzania, Zuchu ameendelea kuandika historia mpya kwenye muziki wake na hii ni baada ya kutajwa kwenye orodha ya vijana wa kiafrika wenye ushawishi zaidi Afrika.
Taarifa hiyo inakuja siku chache tangu video ya Sukari kutoka kwa Zuchu kufikisha views Milioni 100 ikiwa ni video ya kwanza kwa msanii wa kike Afrika kutazamwa mara nyingi zaidi Youtube.
Kwenye orodha hiyo ambayo imeandaliwa na Avance Media, Zuchu ametajwa pamoja na wasanii wengine wakubwa wa kike Afrika ikiwemo mshindi wa tuzo za Grammy, Tayla pamoja na msanii kutokea lebo ya Mavin Ayra Starr.
Wema Sepetu na Zuchu ni watanzania pekee waliyotajwa kwenye orodha hiyo ambayo pia imewataja wasanii wengine kama Davido, Burna Boy, Stone Bwoy kutokea Ghana na msanii Rema kutokea Nigeria
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Diso Ziod
21 April
- Lesson
20 April
- Drop new song loyo
21 April




Leave your comment