Diamond Aingia Kwenye Orodha Ya Wasanii Wenye Tuzo Nyingi Zaidi Afrika

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Diamond Platnumz ameendelea kushika kasi kwenye uwanja wa muziki barani Afrika na hii ni baada ya hivi karibuni kutajwa kwenye orodha ya wasanii wenye tuzo nyingi zaidi Afrika.

Kwenye orodha hiyo ambayo wasanii wengi ni wa Nigeria, msanii Wizkid anaongoza kwa kuwa na tuzo takriban 157 akifuatiwa na Angelique Kidjo mwenye tuzo takriban 140 huku Sarkodie akishika nafasi ya 3 akiwa na tuzo takriban 118.

Kwenye orodha hiyo, Diamond ndiye msanii pekee kutokea Afrika Mashariki kutajwa kwenye orodha hiyo akikadiriwa kuwa na tuzo takriban 70.

Wasanii wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Burna Boy, Davido pamoja na Tiwa Savage.

Leave your comment