Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Gigy Money Afichua Kiasi Alicholipwa Na Harmonize Kwenye Video Ya "Dharau"
25 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Kama umeshaitazama lyrics video mpya ya Dharau kutoka kwa Ibraah akiwa amemshirikisha Harmonize, basi bila shaka ulimuona msanii na socialite maarufu kutokea Tanzania, Gigy Money.
Hivi karibuni, Gigy amefichua kuwa Harmonize alimlipa kiasi cha Tshs Milioni 5 ili aweze kushiriki kwenye video hiyo.
Gigy Money alifichua kuwa, kwa mara ya kwanza alipendekeza kulipwa Milioni 10 lakini mwisho wa siku walikubaliana mpaka Milioni 5.
"Alinipa (Harmonize) Milioni 5 kwa ile shot. Which nilitaka Milioni 10 lakini akaniambia Gigy kwa nyimbo gani, nyimbo yenyewe lyrics video, shot yenyewe moja ya kwenye gari" alizungumza Gigy Money
Gigy Money ni moja ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye muziki nchini Tanzania akiwa na vibao kadhaa kama "Saubona" "Dharau" na nyinginezo nyingi.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Mdundo new features
12 May
- New song
11 May
- My gratitude to my funs
13 May




Leave your comment