Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
"Sukari" Ya Zuchu Yafikisha Views Milioni 100 Kwenye Mtandao Wa YouTube
25 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Msanii nguli kunako kiwanda cha Bongo Fleva, Zuchu hivi karibuni ameandika historia mpya kwenye muziki mara baada ya ngoma yake ya "Sukari" kutazamwa mara Milioni 100 kwenye mtandao wa YouTube.
Ngoma ya "Sukari" iliingia rasmi sokoni Januari mwaka 2021 inakuwa ni ngoma ya kwanza kutoka kwa msanii wa kike Afrika Mashariki kufikisha views Milioni 100 kwenye mtandao huo.
Aidha ngoma ya "Sukari" imeweka rekodi ya kuwa ngoma ya kwanza Tanzania ambayo imefanywa na msanii bila collabo, kufikisha views Milioni 100.
Katika kusheherekea, rekodi hiyo Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram alimshukuru producer Trone na Lizer kwa kutayarisha ngoma hiyo na kuongeza kwa kumshukuru Bosi wa WCB Diamond Platnumz kwa kumuamini.
Kando na Sukari, ngoma nyingine kutoka Tanzania ambazo zimefikisha views Milioni 100 ni pamoja na Waah, Inama na Kwangwaru.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Diso Ziod
21 April
- Lesson
20 April
- Drop new song loyo
21 April




Leave your comment