"B Hitz Was Crazy" Hermy B Agusia Kuhusu Ujio Mpya Wa Bxtra Records

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Mtayarishaji nguli wa muziki kutoka Tanzania, Hermes Joachim maarufu kama Hermy B, hivi karibuni amegusia kuhusu lebo yake ya B Hitz ambayo ilikuwa ni moja kati ya lebo kubwa za muziki nchini Tanzania.

Hermy B ambaye kwa sasa ni CEO wa Bxtra Records amegusia kuhusu lebo hiyo hivi karibuni kupitia uwanja wake wa Instastory.

B Hitz ilikuwa ni lebo ya muziki ambayo ilikuwa inasimamia kazi za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva ikiwemo Gosby, Vanessa Mdee na Mabeste. 

Mwaka 2022, Hermy aliirudisha tena B Hitz kwa kuipa jina jipya la Bxtra Records huku lebo hiyo ikiwa inasimamia kazi za wasanii kama Meja Kunta, Country Wizzy na Jaivah. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram upande wa Instastory, Hermy B akiwa anajibu chapisho kutoka Simulizi Na Sauti ambalo lilikuwa linaenzi kazi za zamani za Vanessa Mdee, producer huyo aliandika kuwa B Hitz ilikuwa nzuri lakini Bxtra Records imekuwa bora zaidi

"B Hitz was crazy but Bxtra Is Amazing" aliandika Hermy B kupitia ukurasa wake wa Instastory, chapisho ambalo lilithibitisha kuwa B Hitz imebadilishwa na kuwa Bxtra Records. 

Hermy B pia ni producer wa ngoma mbalimbali za Bongo Fleva ikiwemo "Zigo Remix", "Habari Ndiyo Hiyo", "Kina Kirefu", "Naongea Na Wewe" na nyinginezo nyingi.

Leave your comment