Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Uchambuzi: Jux Aturudisha Miaka Ya Nyuma Kwenye Ngoma Yake Mpya "Bado"
22 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Kama ulikuwa unapenda ngoma za Jux za zamani kama "Nitasubiri" "Sisikii" au "Uzuri Wako" basi bila shaka utaipenda ngoma yake mpya ya kuitwa "Bado"
Kwenye ngoma yake hii mpya ambayo ni ya tatu kutoka kwake kwa mwaka 2024, Jux anaturudisha kwenye kipindi ambacho alikuwa amejikita zaidi kwenye muziki wa RnB.
Kwenye "Bado" Jux anachanganya ladha ya RnB na Bongo Fleva ili kufikisha ujumbe wake wa mapenzi ambapo ndani ya ngoma hii Jux anasikitika na kuonesha namna ambavyo ameumizwa na mapenzi.
Hii ni ngoma ya 15 kati ya Jux na producer wa muziki Bob Manecky. Wawili hao pia wamehusika kuandaa ngoma tofauti tofauti ikiwemo "Zaidi" "Nakuchana" "Fimbo" na nyinginezo nyingi.
https://youtu.be/fR60_EONQlM?si=miy5wWIbJzz4_5Te
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Domestic Melodies (DM)
29 March
- Free beat
29 March
- Playlist my upcoming song
30 March




Leave your comment