Diamond Na Rayvanny Wazidi Kuwaburuza Burna Boy Na Wizkid Kwenye Mtandao Wa YouTube

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga

Wasanii wawili kutoka Tanzania, Diamond Platnumz na Rayvanny wameendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube wakiwaacha nyuma wasanii kutoka nchini Nigeria. 

Kwenye ripoti ya hivi karibuni, Diamond na Rayvanny wamesimama kama wasanii kutoka Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi YouTube. 

Diamond anaongoza akiwa namba moja na wafuasi takriban Milion 8.7 akifuatiwa na Rayvanny mwenye wafuasi takriban Milioni 4.9 

Orodha hiyo pia ina wasanii wengine wawili kutoka Tanzania ambao ni Harmonize anayeshika nafasi ya 4 na Zuchu anayeshika nafasi ya 8, akiwa ni mwanamke pekee kwenye orodha hiyo. 

Kwa upande wa Nigeria, Burna Boy anashika nafasi ya 3, Davido nafasi ya 7 huku Wizkid akiwa nafasi ya 10

Leave your comment