TID Na Q Chief Wadokeza Ujio Wa Collabo Yao Hivi Karibuni

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Wakali wa muziki wa Bongo Fleva, TID na Q Chief hivi karibuni wamedokeza ujio wa ngoma yao ya pamoja hivi karibuni.

Taarifa kuhusu baina ya wasanii hao imezua zengwe la furaha baina ya mashabiki hasa wale wanaopenda Bongo Fleva za miaka nyuma, kipindi ambacho TID na Q Chief walikuwa wanafanya vizuri.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa TID, legend huyo wa muziki wa Tanzania aliandika kuwa kundi la Top Band Reunion ambalo linamhusisha yeye na Q Chief litaingiza sokoni ngoma yao ya kwanza wiki ijayo na kuongeza kuwa huenda wakaachia album hivi karibuni. 

"Top Band Reunion New Single Is Coming Next Week Hatuna Band Ya Kutuzuia Kufanya Album So Mkae Mkao Wa Kula" aliandika TID ambaye kupitia chapisho lake.

Ikumbukwe kuwa TID na Q Chief walikuwa kwenye mgogoro kwa miaka kadhaa sasa na kwamba collabo hii inatarajiwa kuwa mwanzo mpya wa kisanaa baina ya wawili hao.

Leave your comment