Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Producer S2kizzy Athibitisha Kufanya Ngoma Na Msanii Wa Nigeria, Patoranking
19 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Bila shaka mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania S2kizzy yuko katika harakati za kupeleka sanaa yake duniani na hii ni baada ya producer kudokeza kufanya kazi mpya na msanii kutokea Nigeria Patoranking.
S2kizzy amedokeza kuhusu ujio wa project hiyo na Patoranking katika kipindi ambacho ngoma zake mbili ambazo ameziandaa yaani Daah ya Nandy na Mapoz ya Diamond Platnumz zinafanya vizuri.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, S2kizzy alipoat video akiwa na msanii Patoranking studio wakirekodi ngoma pamoja, jambo ambalo limepelekea mashabiki wengi kuwa na hamu ya kusikiliza collabo hiyo pindi itakapotoka.
S2kizzy ni mtayarishaji wa muziki kutokea Tanzania ambaye ngoma zake kama "Nitongoze" ya Rayvanny, "Komando" ya G Nako Na Diamond Platnumz, "Shisha" Ya Marioo na nyinginezo nyingi zimepelekea yeye kuwa moja ya watayarishaji wakubwa wa muziki Afrika.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Free beat
29 March
- Domestic Melodies (DM)
29 March
- Playlist my upcoming song
30 March




Leave your comment