Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Country Wizzy Aandika Rekodi Mpya Nchini Tanzania Kwenye Mtandao Wa YouTube
19 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Rapa kutokea Tanzania ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya kuitwa Way Back amefikisha idadi mpya ya wafuasi au subscribers kwenye akaunti yake YouTube.
Country Wizzy hivi karibuni amefikisha idadi ya subscribers laki mbili kwenye akaunti ya YouTube na hivyo kupelekea rapa huyo kuwa kwenye orodha ya wasanii wa Hip Hop nchini Tanzania wenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao huo
Kwa sasa Wizzy anashika namba 8 kwenye orodha ya rappers wenye subscribers wengi zaidi Tanzania baada ya Darassa, Nay Wa Mitego, Roma Mkatoliki, Dogo Janja, Professor Jay, Billnass na wengineo wengi.
Country alianzisha akaunti yake ya YouTube mwaka 2012 na mpaka sasa ana jumla ya views zaidi ya Milioni 10 kwenye akaunti yake ya YouTube.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Free beat
29 March
- Domestic Melodies (DM)
29 March
- Playlist my upcoming song
30 March




Leave your comment