D Voice Afunguka Baada Ya Zuchu Kufungiwa Kufanya Muziki

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli kutokea kiwanda cha muziki Tanzania, D Voice hivi karibuni amefunguka kufuatia msanii mwenzake kutokea lebo ya WCB, Zuchu kufungiwa kufanya muziki huko Visiwani Zanzibar.

Siku chache zilizopita, Zuchu ambaye kwa sasa anatamba na mkwaju wake wa kuitwa Zawadi, alifungiwa kufanya muziki huko visiwani Zanzibar kwa muda wa miezi 6 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kutoa matamshi yasiyofaa na ambayo ni kinyume na maadili ya Kizanzibari mnamo Februari 24 mwaka huu wakati Zuchu akitumbuiza katika tamasha la Fullmoon huko Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Akizungumza hivi karibuni, D Voice amedokeza kuwa hata yeye amepata funzo baada ya adhabu hiyo ya Zuchu na kuongeza kuwa kuna muda serikali iwawie radhi pindi wakiwa wanatumbuiza jukwaani. 

"Viongozi wetu pia wanaotusimamia wanatakiwa waelewe, watuwie radhi kwa sababu mtu unapopanda pale unakuta vibe kwa hiyo lolote linaweza kunitoka." alizungumza D Voice 

Nnachozingatia tu muziki wangu uwe na nidhamu, nisivuke mipaka lakini kuna muda unajikuta kwamba vibe imezidi" alizungumza D Voice

Leave your comment