Collabo Ya D Voice Wa WCB Na Vanillah Wa Kings Music Iko Mbioni? D Voice Afunguka

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Baada ya uwepo kwa minong'ono ya muda mrefu kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa collabo baina ya D Voice na Vanillah, hatimaye hivi karibuni D Voice amefunguka kuhusu taarifa hizo.

Siku chache zilizopita D Voice na Vanillah walitikisa mitandao ya kijamii mara baada ya video inayowaonesha wakiwa gym na kutaniana kusambaa mitandaoni na kupelekea mashabiki kudhani kuwa huenda wawili hao wana ngoma ya pamoja.

Akizungumza hivi karibuni, D Voice ambaye alitambulishwa kama msanii rasmi wa WCB Wasafi mwezi Novemba mwaka 2023 alisema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Vanillah kama biashara na uongozi wake utaruhusu.

"Kama itatokea kuna ngoma tunaweza tukaua, kuna ngoma ambayo nahisi nikapita vizuri na threat kwa sababu sisi ni wasanii na muhimu ni biashara" alizungumza D Voice.

D Voice aliongeza kwa kusema " Muhimu tu ni biashara, kama biashara yangu inaruhusu na uongozi wangu pia unaruhusu tunafanya"

 

Vanillah ni msanii wa Kings Music ambayo ni lebo ya Ali Kiba ambaye anajulikana kwa ngoma zake kama "For You" na "Unanisitiri"

Leave your comment