Zuchu Na Marioo Wachukua Likizo Kutumia Mtandao Wa Instagram

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Wasanii nguli kutoka Tanzania, Marioo na Zuchu hivi karibuni wameingia kwenye vichwa vya vyombo vya habari nchini na hii ni baada ya wasanii hao kuchukua likizo ya kutumia mtandao wa Instagram. 

Marioo kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha ujumbe unaoonesha kuwa ukurasa wake wa Instagram uko kwenye "matengenezo" na hivyo kudokeza kuwa kwa hatakuwepo kwa muda kwenye mtandao huo.

Zuchu kwa upande wake ameonekana kuipumzisha akaunti yake ya Instagram  kwani kwa sasa hakuna post yoyote inayoonekana kwenye akaunti hiyo ambayo ina mamilioni ya wafuasi 

Mara baada ya mastaa hao kuchukua uamuzi huo, mashabiki wengi wamedokeza kuwa huenda uamuzi wa mastaa hao ni kwa sababu ya uwepo wa mfungo wa mwezi Ramadhan na pengine mara baada ya mwezi huu kuisha basi watarudi kwenye mtandao huo.

Leave your comment