Diamond, Ali Kiba na Harmonize Watajwa Kwenye Orodha Ya Wasanii Wanaolipwa Zaidi Afrika

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Wasanii wanne kutoka Tanzania Diamond Platnumz, Ali Kiba, Harmonize na Rayvanny wametajwa na mtandao wa Africa Facts Zone kwenye orodha ya wasanii ambao wanaolipwa zaidi barani Afrika. 

Africa Facts Zone walitoa orodha hiyo kwa lengo la kuonesha ni wasanii gani kutokea barani Afrika wanalipwa pesa nyingi zaidi wakiitwa kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki. 

Orodha hiyo inaongozwa na msanii Burna Boy, Wizkid na David kutoka nchini Nigeria wao wanatoza $1 million ambazo ni sawa na 2.5 Billions Tshs wakati Diamond Platnumz anashika nafasi ya 14 kwenye orodha hiyo yeye akitoza $100000 ambazo ni sawa 255M Tshs. 

Ali Kiba kwa upande wake anatoza $50000 ambazo ni sawa 127M Tshs, Harmonize yeye anatoza $25000 ambazo ni sawa na 63M huku Rayvanny yeye anatoza $20000 ambazo ni sawa na 51M Tshs.

Kwenye orodha hiyo hakuna msanii yeyote wa Hip Hop kutoka Tanzania aliyetajwa

 

Leave your comment