"Nilidanganya Kuhusu Collabo Yangu Na Maluma" Rayvanny Adokeza

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Hivi karibuni msanii nguli kutoka Tanzania, Rayvanny alidokeza kuwa alitumia ujanja na kuongopea mashabiki mpaka kupata collabo yake na msanii maarufu kutoka Columbia Maluma. 

Akiongea kwenye podcast ya 3 Shots Of Tequila, Rayvanny alidokeza kuwa muda mfupi baada ya kuona Maluma ameimba ngoma yake kupitia Instagram aliamua kumfuata msanii huyo DM kwa ajili ya kuomba collabo lakini msanii huyo hakujibu. 

Rayvanny ambaye pia ni mshindi wa BET aliongeza kwa kusema kuwa baada ya kuona DM yake haijajibiwa na Maluma, aliamua kuchapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba ana collabo na Maluma ingawa walikuwa hawajakubaliana, kitendo ambacho kilisababisha media zote ziandike kuhusu collabo na hivyo kupelekea Maluma kuona muhimu wa collabo hiyo na hatimaye wakashirikiana. 

“Nilikuwa nimeona video moja ya Maluma akiwa LA nadhani alikuwa anafurahi ngoma yangu na nikaona hii ni fursa. Nikamtuma message lakini hakujibu. Nikawaza ni kitu gani ambacho naweza nikafanya ili anione” aliongeza Rayvanny 

Rayvanny aliongeza kwa kusema “Kwa hiyo nilienda kupost mimi na Maluma tuna ngoma ya pamoja na itatoka hivi karibuni na nilikuwa nadanganya. Kwa hiyo blogs zote na media zikaanza kunipost mimi na yeye na hatimaye alinitumia ujumbe” 

 

 

 

 

 

Leave your comment