Dayoo Afunguka Usiyoyajua Kuhusu Collabo Yake Na Msanii Asake

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Mtunzi na mwandishi wa ngoma ya Huu Mwaka, Dayoo hivi karibuni amedokeza kuhusu uwezekano uliopo wa yeye kufanya kazi na msanii kutokea Nigeria, Asake. 

Tamko hili la Dayoo linakuja siku chache tangu msanii huyo ambaye anajulikana kwa ngoma zake kali ikiwemo ”Nikuone” kuchapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram mazungumzo baina yake na Asake kuhusu ujio wa ngoma yao ya pamoja. 

Hivi karibuni, Dayoo alidokeza kuwa aliamua kufuta chapisho hilo baada ya mashabiki kumshauri kuwa kuwa si vyema yeye kuvujisha mazungumzo nyeti kama hayo na kuongeza kuwa kuna baadhi ya wadau wakubwa wa muziki pia walimfuata kumwambia kuwa si vyema yeye kuweka mazungumzo hayo hadharani. 

“Ile post ilikuwa imeenda trending sana. Nikafatilia comments nyingi ni watu wa Nashauri usipende kupost vitu vyako hadharani lakini pia kuna baadhi ya brothers wakubwa walinushauri pia so nikaona sio kitu sahihi kubaki kwenye akaunti yangu” alizungumza Dayoo 

Dayoo aliongeza kwa kusema “Hata hapo mi nadhani tuiache iendelee kukata private mpaka pale siku itakapotokea” 

 

Leave your comment