“Mengi Yatasemwa” Baba Levo Afunguka Baada Ya Ali Kiba Kufungua Redio Yake

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii na mtangazaji nguli kutokea nchini Tanzania, Baba Levo hivi karibuni ametoa pongezi kwa msanii mwenzake Ali Kiba ambaye hivi karibuni amefungua kituo chake cha redio, Crown FM pamoja na kituo cha Televisheni Crown TV. 

Siku chache zilizopita Ali Kiba akiwa kwenye hafla ya kusherehekea miaka 20 ya kuhudumu kwenye kiwanda cha muziki, alitangaza kuwa amefungua kituo cha redio, Crown FM pamoja na kituo cha televisheni, Crown TV. 

Akizungumza hivi karibuni, Baba Levo amempongeza Ali Kiba kwa kufungua kituo cha redio na kusema kuwa ni jambo zuri kwani ni uwekezaji wenye tija. 

“Redio mpya ya Ali Kiba ni kitu kizuri, mtu kuwekeza kwenye biashara kwa sababu muziki una mwisho wake. So kuwekeza kwenye redio ni vizuri japokuwa mengi yatasemwa lakini all in all hata kama ana share lakini share kama anayo ni mmiliki” alizungumza Baba Levo. 

Kando na Ali Kiba, msanii mwingine kutoka Tanzania ambaye anamiliki redio na TV ni Diamond Platnumz ambaye yeye ni mmiliki wa Wasafi TV na Wasafi FM, vyombo vya habari ambavyo kwa sasa vinafanya vizuri. 

 

Leave your comment