Rayvanny Atia Neno Kuhusu Kufanya Kazi Na Msanii Adele

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga

Download New Kalenjin DJ Mixes on Mdundo

Nyota wa muziki kutoka Tanzania, Rayvanny hivi karibuni amemtaja Adele kutokea Uingereza kama moja ya wasanii wakubwa ambaye angependa sana kufanya nae kazi. 

Rayvanny ameyasema hayo hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano kwenye podcast ya “3 Shots Of Tequila” huko Uingereza. 

Kwa sasa Rayvanny yuko barani Ulaya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki ambapo wiki chache nyuma alikuwa nchini Ufaransa na kwa sasa ametua Uingereza. 

Akiwa anajibu swali la moja ya watangazaji wa podcast hiyo maarufu duniani, Rayvanny alianza kwa kudokeza kuwa angependa kufanya kazi na wasanii wawili ambao ni Justin Bieber na Ed Sheran lakini katika mazungumzo hayo alimuongeza Adele na kusema kuwa kwake yeye, Adele ndio msanii namba moja ambaye angependa kufanya nae kazi. 

Adele ni msanii wa miondoko ya pop kutokea nchini Uingereza ambaye anakadiriwa kuwa na mauzo ya takriban nakala Milioni 120 tangu aanze muziki na anajulikana kwa ngoma zake tofauti tofauti ikiwemo “Someone Like You” “Easy On Me” “Hello” na nyinginezo nyingi. 

 

 

 

Leave your comment