Billnass Na Mbosso Waonesha Uhalisia Wa Aina Yake Kwenye Video Mpya Ya "Number One"

 

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Rapa kutoka Tanzania Billnass hatimaye ametimiza ahadi yake kwa mashabiki baada ya kuachia video ya ngoma yake ya kuitwa “Number One” ambayo amemshirikisha msanii kutokea lebo ya WCB Wasafi, Mbosso. 

Video ya “Number One” inakuja siku chache tangu Billnass aachie audio ya ngoma hiyo ya mapenzi ambayo ina mahadhi ya Bongo Fleva, Baibuda pamoja na muziki wa Hip Hop. 

Ndani ya video ya “Number One” Mbosso na Billnass ameonesha uhalisia wa aina yake ambapo Mbosso ameigiza kama mwanaume mtafutaji ambaye anatumia mbinu tofauti tofauti kujikwamua na bila shaka stori nzima ya video itakosha mashabiki wengi sana. 

Video hii imefanyika huko jijini Arusha Tanzania na imeongozwa na Director Folex ambaye pia amehusika kutayarisha video za wasanii tofauti tofauti ikiwemo "Daah" ya Nandy akiwa na Ali Kiba, "Bam Bam" ya D Voice na "Enjoy" ya Juma Jux na Diamond Platnumz. 

https://youtu.be/GGuBo-is2XM?si=RFylsmG0LZsD20oj

Leave your comment