Ali Kiba, Country Wizzy Na Wasanii Wengine Wa Tanzania Walioachia Ngoma Mpya Wiki Hii

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Wasanii kutoka Tanzania ikiwemo Darassa, Ali Kiba, Country Wizzy na wengineo kwa mara nyingine wameweza kuchakata bidhaa bora za muziki kwa lengo la kuburudisha mashabiki zao. 

Hizi ni hapa ngoma mpya nchini Tanzania kwa wiki hii: 

 

Way Back - Country Wizzy Ft Jay Moe 

Baada ya kuachia Current Situation miezi kadhaa nyuma, rapa Country Wizzy amerudi na "Way Back", ngoma kali yenye ujumbe wenye lengo la kutoa faraja na kuburudisha na ambayo ndani amemshirikisha Jay Moe

 

Huku Remix - Tommy Flavour & Ali Kiba Ft Iyanya 

Katika harakati za kuipeleka Bongo Fleva kimataifa, Ali Kiba na Tommy Flavour wameungana na Iyanya kuileta "Huku Remix" kwenye masikio ya wasikilizaji ambao bila shaka wameipokea ngoma hii kwa mkono miwili. 

Wanawake Moto - Samia Queens 

Kwenye ngoma hii wasanii tofauti tofauti wa kike kutoka Tanzania ikiwemo Zuchu, Maua Sama, Nandy, Queen Darleen na wengineo wengi wameungana pamoja kuonesha mchango wa mwanamke katika jamii. 

No Time - Darassa Ft Jux 

Kama unapenda michano kutoka kwa  Darassa basi bila shaka pia utaipenda ngoma hii mpya ya kuitwa "No Time" ambayo ndani yake Darassa amefanya na Jux ambaye sauti yake mujarab imeipamba ngoma hii ambayo kwa sasa unatamba kwenye mitaa tofauti nchini Tanzania. 

Niambie - Mac Voice 

Ukimya wa Mac Voice kwenye kiwanda cha muziki ulileta taharuki kwa wapenda muziki lakini wiki hii, kinda huyo aliachia “Niambie” ngoma kali ya mapenzi yenye mahadhi ya Bongo Fleva, ambayo imevunja ukimya wake kwenye muziki. 

 

 

 

 

Leave your comment