Mac Voice Wa Rayvanny Arudi Kivingine Na Ngoma Mpya "Niambie"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya ukimya wa miezi kadhaa, hatimaye msanii kutokea lebo ya Next Level Music ya kwake Rayvanny, Mac Voice ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa "Niambie" 

Kwa wapenzi wa ngoma za mapenzi na zenye mahadhi ya kubembeleza basi ngoma hii ya kuitwa “Niambie” ni mahsusi kwa ajili yao, ngoma hii ikiwa ni ngoma ya kwanza kutoka kwa Mac Voice kwa mwaka 2024. 

Kwenye “Niambie” Mac Voice ambaye mwezi Oktoba mwaka 2022 alitajwa kuwania kipengele cha msanii bora chipukizi kwenye tuzo za AEAUSA ametumia mahadhi ya Bongo Fleva kwenye ili kufikisha ujumbe wake, ladha ya muziki ambayo pia alitumia kwenye ngoma yake ya "Nenda" na "Sikuachi." 

"Niambie" imetayarishwa na Sound Boy, ambaye ni producer rasmi wa lebo ya Next Level Music ambayo ni ya msanii Rayvanny 

https://youtu.be/HthfRK0Idww?si=gNFLWaHO20iT6zJp

Leave your comment