Country Wizzy Aungana Na Jay Moe Kwenye Ngoma Ya "Way Back"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga

Msanii nguli kutoka kiwanda cha muziki nchini Tanzania, Country Wizzy hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa "Way Back" ambayo amemshirikisha Jay Moe.

Kwenye "Way Back" Country Wizzy anazungumzia kuhusu maisha na jinsi ambavyo amepitia changamoto mbalimbali kwenye maisha bila kukata tamaa.

Jay Moe kwa upande amepamba kibao hiki kwa michano yake iliyoshiba na ambayo imejaa uhalisia wa maisha.

Ammy Wave ndiye amehusika kuandaa ngoma hii akiwa pia ni producer ambaye amehusika kuandaa kazi za wanamuziki mbalimbali Tanzania

Sikiliza Way Back Hapa:

https://youtu.be/4IpogTkP0d0?si=KOfx7xJBi_rg_esd

Leave your comment