"Walitoka Kwa Majigambo" K2ga Agusia Maisha Ya Killy Na Cheed Baada Ya Kuondoka Kings Music

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii kutokea lebo ya Kings Music K2ga hivi karibuni amezungumzia sakata la wasanii wawili, Killy na Cheed kuondoka kwenye lebo ya Ali Kiba, Kings Music. 

K2ga amezungumzia sakata hilo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu wasanii hao “kupotea” kwenye muziki baada ya kuondoka kwenye lebo ya Konde Music Worldwide ya kwake Harmonize. 

Killy na Cheed walitangazwa kuondoka kwenye lebo ya Konde Music Worldwide mwezi Oktoba 2022 na kabla ya hapo wasanii hao wawili walikuwa chini ya lebo ya Kings Music ya kwake Ali Kiba. 

Akizungumza hivi karibuni, K2ga alidokeza kuwa huenda wasanii hao hawafanyi vizuri kwa sasa kwani baada ya kuondoka kwenye lebo ya Kings Music walizungumza kwa majigambo sana na kwamba kitendo cha wao kutaja changamoto walizokuwa wanapitia wakiwa kwenye lebo hiyo imepelekea wao kutofanya vizuri kwa sasa. 

“Walichofeli mara ya kwanza ni kutoka kwa majigambo, kwa kuitangaza zile shida walizofanya watoke. Hicho ndo walichokosea. Lakini kama wangetoka tu alafu wange-mute wafanye mambo yao mengine ingekuwa sawa sana.” alizungumza K2ga. 

 

 

 

 

 

Leave your comment