Billnass Afichua Sababu Ya Mbosso Kukosekana Kwenye Lyrics Video Ya Ngoma Yake Ya "Number One"

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Msanii wa Hip Hop kutokea kiwanda cha muziki nchini Tanzania, Billnass hivi karibuni amefunguka kufuatia msanii kutokea WCB, Mbosso kukosekana kwenye lyrics video ya ngoma ya Number One ambayo amemshirikisha. 

Billnass na Mbosso hivi karibuni walitetemesha kiwanda cha muziki Tanzania baada ya kuachia ngoma ya kuitwa “Number One”. Ngoma hiyo ilisindikizwa na Lyrics video ambayo ndani yake Mbosso hakuonekana badala yake alionekana Billnass peke yake. 

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano, Billnass alisema kuwa Mbosso hakupata nafasi ya kuwepo kwenye Lyrics video hiyo kwani Mbosso alikuwa kwenye ziara huko nchini Canada wakati yeye anaandaa video hiyo na hivyo kupelekea ratiba zao kuingiliana. 

“Kwenye Lyrics Video ilikuwa ngumu Mbosso kuonekana kwa sababu kama unavyojua Mbosso yeye alikuwa na safari ya Canada na hiyo siku ambayo mi nilikuwa na-shoot kama kesho yake yeye ndo alitakiwa kuwa anaenda Canada na mimi nilikuwa na-shoot South Africa” alizungumza Billnass. 

Kando na Mbosso, tangu aanze muziki takriban miaka 8 iliyopita, Billnass ameshafanya kazi na wasanii wengine tofauti tofauti ikiwemo Mwana FA, Marioo, Jay Melody, Nandy na wengineo wengi. 

 

Leave your comment