Zuchu Aomba Radhi Baada Ya Kufungiwa Kufanya Muziki

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Saa chache baada ya BASATA kumfungia msanii Zuchu kufanya kazi za sanaa kwa miezi 6, msanii huyo kutoka lebo ya WCB amejitokeza hadharani na kuzungumzia sakata hilo. 

Zuchu siku ya jana alifungiwa kufanya shughuli za sanaa kisiwani Zanzibar kwa muda wa miezi 6 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutoa matamshi ambayo ni kinyume na maadili ya kizanzibari mnamo Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Hivi karibuni, msanii huyo amejitokeza na kuomba radhi kutokana na matamshi aliyoyatoa na kuongeza kuwa alikuwa lengo lake kuudhi watu badala yake alikuwa na lengo la kuburudisha tu. 

“Hivyo basi kutokana na sintofahamu iliyojitokeza tarehe 24 kwenye show yangu ya Zanzibar pale Kendwa niombe radhi kwa jamii kama Kuna sintofahamu imejitokeza na kama mtu yeyote au kuna mlengwa yeyote imemkera. Lengo lilikuwa ni kuburudisha na sio kupotosha mahala” alizungumza Zuchu. 

 

Leave your comment