Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Tommy Flavour Na Ali Kiba Wamshirikisha Iyanya Kwenye "Huku Remix"
6 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Kama ulikuwa umeisubiri kwa muda mrefu basi habari njema ni kwamba tayari Tommy Flavour na Ali Kiba ameachia remix ya ngoma yao ya Huku ambayo wamemshirikisha msanii kutokea nchini Nigeria, Iyanya.
Ngoma ya Huku Remix inakuja wiki chache tangu Kings Music, lebo inayomilikiwa na msanii Ali Kiba kudokeza ujio wa ngoma hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
Toleo la kwanza la ngoma ya "Huku" liliingia sokoni takriban miezi mitano iliyopita na kupokelewa vyema sana na mashabiki ambapo mpaka sasa video ya ngoma hiyo imeshatazamwa takriban mara Milioni 6 kwenye mtandao wa YouTube.
Kwenye Huku Remix, Iyanya ameongeza ladha ya Afrobeats kwenye ngoma hiyo yenye miondoko ya Bongo Piano ambapo kupitia verse yake, msanii huyo kutokea nchini Nigeria ameongeza vionjo vya lugha ya kiingereza na kuifanya ngoma hii kunoga zaidi.
Kwa collabo hii, Ali Kiba anakuwa ni msanii wa pili kutoka Tanzania kufanya collabo na Iyanya baada ya Diamond Platnumz ambaye miaka 10 iliyopita alifanya kazi na Iyanya kwenye ngoma mbili ambazo ni “Bum Bum” pamoja na “Nakupenda”
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Free beat
29 March
- Playlist my upcoming song
30 March
- ITSLILREMY
30 March
- Usman Khalifa Amoto
30 March




Leave your comment