"Siwezi Kufanya Show Chini Ya Milioni 10" Baba Levo Adokeza

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Mtangazaji na msanii nguli kutokea kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania, Baba Levo hivi karibuni amevuta hisia za mashabiki wengi baada ya hivi karibuni kusema kuwa hawezi kufanya show bila kulipwa Milioni 10. 

Baba Levo ambaye pia anafahamika kwa kuwa shabiki mkubwa wa msanii Diamond Platnumz ametoa kauli hiyo hivi karibuni. Baba Levo anajulikana kwa ngoma zake mbalimbali ikiwemo Hellow, Baikoko na nyinginezo nyingi. 

Akizungumza hivi karibuni kwenye kipindi cha Mgahawa, Baba Levo alidokeza kuwa kwa sasa hawezi kukubali kufanya show au kutumbuiza sehemu yoyote bila kulipwa Milioni 10. 

“Sifanyi show kwa sababu moja. Nadhani nimejiwekea bei kubwa. Sifanyi show chini ya Milioni 10.” alizungumza Baba Levo. 

 

 

 

 

 

 

 

Leave your comment