Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Rapa Msamiati Afunguka Jinsi Alivyomvuta Conboi Kwenye "Tumeondoka"
2 March 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Kama unafuatilia kiwanda cha muziki kutoka Tanzania basi bila shaka utakuwa unafahamu kwamba “Tumeondoka” ya rapa Msamiati, ni moja kati ya ngoma chache za Hip Hop zinazofanya vizuri zaidi nchini.
Audio ya Tumeondoka ambayo iliingia sokoni takriban miezi 6 iliyopita, imesindikizwa na video mpya na kali ambayo imeachiwa siku nne zilizopita na mpaka sasa video hiyo ikiwa imeingia kwenye “Trending” ya YouTube 
Kwenye ngoma hiyo, Msamiati amemshirikisha Joh Makini na Conboi ambaye amepamba ngoma hiyo na mistari yake mujarab.
Akizungumzia ngoma hiyo, Msamiati alidokeza kuwa alianza kuingia studio na Joh Makini lakini baadaye aliona kwamba kuna pengo na ndipo hapo aliamua kumshirikisha Conboi ili aweze kuipa uzito zaidi ngoma hiyo.
“Baada ya kuwa nimemaliza mziki, nikawa nahisi kuna kitu nakihitaji. Nikawa naona kuna kitu tofauti cha mtu kama Coni. Lakini nilikuwa sijawahi kukutana na Coni. Hatujawahi kukutana actually kwa ajili ya kuzungumza kuhusu kazi”
Video ya Tumeondoka inapatikana sasa kupitia mtandao wa YouTube:
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Mdundo new features
12 May
- My gratitude to my funs
13 May
- Tenacious avenue
13 May
- Yayami
13 May




Leave your comment