Ngoma 3 Ambazo Marioo Ameshawahi Kuandikia Wasanii Wengine

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Ukiweka kando uwezo wake wa kuimba, Marioo pia anajulikana kwa kipaji chake cha kuandika na utunzi mzuri wa ngoma tofauti tofauti zenye mahadhi ya Amapiano, Bongo Fleva na nyinginezo nyingi. 

Akiwa na hits kama Bia Tamu, Dear Ex, Ifunanya, Asante, Lonely na nyinginezo nyingi Marioo pia anasifika kwa kuandika ngoma wasanii wengine. 

Kutoka kwa wasanii kama Gigy Money , Nandy na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma 3 ambazo Marioo ameshawahi kuandikia wasanii wengine: 

 

Papa - Gigy Money 

Papa ya Gigy Money iliandikwa na Marioo na bila shaka huu ni wimbo mkubwa zaidi kwa Gigy Money tangu aanze mitikasi ya muziki na kupitia ngoma hii ambayo iliingia sokoni mwaka 2017, Marioo aliweza kuwa maarufu zaidi. 

 

Wasikudanganye - Nandy 

“Wasikudanganye” ambayo iliingia sokoni mwaka 2017 ni moja kati ya ngoma kubwa kutoka kwa Nandy lakini ukweli ni kwamba ngoma hii pia iliandikwa na Marioo ambaye aliichora ngoma hii kipindi bado hajawa maarufu kama alivyo sasa. 

 

Nabembea - Ditto 

Msanii Ditto anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kuandika mashahiri lakini kwenye “Nabembea” Ditto alimpa nafasi Marioo ya kuandika wimbo huo ambao kutokana na mashahiri mazuri yalioandikwa na Marioo, ngoma hiyo ilipokelewa vyema sana na mashabiki. 

 

 

 

Leave your comment