Yammi Afunguka Jinsi Nandy Na Zuchu Walivyokutana Studio Pamoja

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii anayefanya vizuri kwa sasa kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Yammi, hivi karibuni amefungua kufuatia kipande cha video kilichokuwa kikisambaa mitandaoni kikiwaonesha Zuchu, Nandy na Yammi wakiwa studio wanarekodi ngoma. 

Mapema mwezi January kupitia mtandao wa Tiktok, video ambayo inawaonesha wasanii mbalimbali wa kike kutoka Tanzania wakiwa wapo studio ilisambaa na kuzua taharuki kwa mashabiki kuhusu nini hasa kinapikwa na wasanii hao. 

Kwenye video hiyo fupi wasanii kama Nandy, Zuchu, Yammi, Khadija Kopa, Anjella na Queen Darleen walionekana wakiwa wapo studio, kitu ambacho kiliashiria kuwa huenda kuna mradi wa muziki unakuja. 

Akizungumza hivi karibuni, Yammi amesema kuwa kwa sasa bado hayupo tayari kuzungumzia nini hasa kilitokea katika video hiyo lakini alidokeza kwamba alijisikia furaha kuwepo kwenye eneo moja na wasanii wenzake wakubwa wa kike ikiwemo Zuchu na Nandy. 

“Ile moment Kwangu ilikuwa ni nzuri nilifurahi nilikutana na wasanii wenzangu mbalimbali. Wengine nilikuwa sijawahi kukutana nao kwa mfano Zuchu kwa hiyo siku ndo nilikutana nae” alizungumza Yammi.

Yammi ni msanii kutoka Tanzania ambaye kwa sasa amesainiwa nchini ya lebo ya The African Princess ya kwake Nandy. Ngoma zake kama Namchukia, Hanipendi na Tiririka zimemfanya kinda huyo kuwa mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

 

Leave your comment