Vanillah Wa Kings Music Afunguka Madai Ya Kuiga Ngoma Ya Otile Brown

 

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya baadhi ya watu kufananisha ngoma mpya ya Vanillah na ngoma ya zamani ya Otile Brown, Vanillah hivi karibuni amezungumzia kuhusu sakata hilo. 

Siku chache zilizopita, Vanillah wa Kings Music aliachia ngoma yake ya kuitwa Body na tangu kuachiwa kwake baadhi ya wadau wameifananisha melody ya ngoma hiyo na ngoma ya Otile Brown akiwa na Ali Kiba ya kuitwa “In Love” 

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano na John Jackson, Vanillah alidokeza kuwa hakufahamu kwamba kuna mfanano baina ya ngoma hizo mbili na kwamba hakuwa na lengo la kuiga miondoko ya ngoma hiyo. 

“Mimi sijagundua (kuna mfanano) inabidi nisikilize kwa sababu hata nimesahau kidogo melody za huo wimbo lakini kama zinafanya kama umeshasikiliza mimi sikumbuki” alizungumza Vanillah. 

Vanillah ni msanii kutokea lebo ya Kings Music ya Ali Kiba na kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Body akiwa na Tommy Flavour. 

 

Leave your comment