Harmonize Atangaza Kusaini Wasanii Wapya Konde Gang

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli kutokea nchini Tanzania, Harmonize hivi karibuni amedokeza kuwa yupo mbioni Kusaini wasanii Wapya kwenye lebo yake ya Konde Music Worldwide al maarufu kama Konde Gang. 

 

Kwa sasa Konde Gang ina wasanii wawili tu ambao ni Harmonize na Ibraah na hii ni baada ya wasanii wengine ambao walikuwa kwenye lebo hiyo kuondoka kutokana na sababu tofauti tofauti. 

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize kwenye ujumbe ambao alikuwa amemuandikia Ibraah alimshukuru Ibraah kwa kumpa moyo wa kuendelea kutengeneza vipaji vipya kwenye Bongo Fleva huku akidokeza kuwa yupo mbioni kusaini wasanii wengine kwenye lebo hiyo. 

“Busara Unyenyekevu Uvumilivu Nibaadhi Ya Vitu Vinamfanya CHINGA Awe Hapa Leo!!!! PROUD OF YOU BROTHER ushauri Wako Naufanyia Kaziii Ingawa Nilikaribia Kukata Tamaa Kabisa Kuwa Support Wasanii Wengine Ila MANENO YAKO YAMENIPA NGUVU UPYA!!!! 2 MEMBERS @kondegang HUU MWAKA !!! 2024” aliandika Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram. 

Wasanii ambao walikuwa ni sehemu ya Konde Gang na Kisha baadae kuamua kuachana na lebo hiyo ni pamoja na Lilly, Cheed, Anjella na rapa Country Wizzy ambaye kwa sasa anahudumu kwenye lebo ya Bxtra Records. 

 

Leave your comment