Jaivah Athibitisha Kumaliza Sintofahamu Yake Na Chino Kidd

 

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii kutokea lebo ya Bxtra Records, Jaivah hivi karibuni amethibitisha kumaliza sintofahamu iliyotokea siku chache zilizopita kati yake na msanii anayekuja kwa kasi kwenye muziki, Chino Kidd. 

Siku chache zilizopita, Jaivah na Chino Kidd waliingia kwenye vichwa vya habari nchini Tanzania baada ya Chino Kidd kudokeza kuwa Jaivah na Marioo hawakumuunga mkono kwenye show yake ya Wanaman Experience pale Warehouse Arena, Masaki. 

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Tanzania, Jaivah amedokeza kuwa yeye na Chino Kidd wako vizuri na wamemaliza Ile sintofahamu iliyotokea baina yao. 

“Sisi wote tuko sawa. Nadhani kama Kuna yeyote alikosea kama ni Chino au Marioo kwa sasa ni yameisha, hakuna tatizo lolote na hakuna mtu yeyote ambaye labda alikuwa anajaribu kuvunja chochote” alizungumza Jaivah.

Jaivah, Marioo na Chino Kidd ni wasanii ambao kwa muda mrefu sasa wamejulikana kwa urafiki wao wa muda mrefu na pia ameshirikiana kwenye ngoma tofauti tofauti ikiwemo Soup pamoja na Yesa. 

 

 

 

 

Leave your comment