Ngoma Mpya Tanzania: Ali Kiba Aachilia ON FIRE


Imange courtesy Instagram

Mwandishi Charles Maganga

Baada ya ukimya wa takriban miezi mitatu hatimaye “Only One King” kunako kiwanda cha Bongo Fleva, Ali Kiba ameachia mkwaju mpya kabisa wa kuitwa “On Fire” 

“On Fire” inakuja siku chache kuelekea kwenye tamasha kubwa la kuitwa “Reloaded” ambapo Ali Kiba atatumbuiza kwenye jukwaa moja na msanii kutokea huko nchini Nigeria wa kuitwa Ayra Starr pale Superdome, Masaki. 

“On Fire” ni ngoma kali ya Bongo Fleva ambayo ndani yake King Kiba anatoa sifa kedekede kwa mpenzi wake ambapo anamsifia mpenzi wake kutokana na urembo alionao. Kama kawaida, Ali Kiba ametumia sauti yake mujarab kupamba mkwaju huu. 

“On Fire” ni ngoma ya tatu  kutoka kwa Ali Kiba kwa mwaka huu baada ya hapo awali kuachia “Mahaba” ambayo imeshakusanya views takriban Milioni 9 kwenye mtandao wa Youtube na “Lalala” ambayo ameshirikiana na wasanii wa Kings Music. 

Leave your comment

Top stories

More News