Video Mpya Ya Mbosso “Amepotea” Inastahili Tuzo 


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii

Ukisikiliza “Amepotea” ni dhahiri shahiri kuwa, Mbosso alikuwa amepania haswaa kuiteka Bongo Fleva na ukienda mbele zaidi kuitazama video ya wimbo huu bila shaka utagundua kwamba Mbosso anajua nini hasa kinahitajika kwa sasa kwenye kiwanda cha muziki.  

Kama unafuatilia muziki wa Bongo Fleva basi bila shaka utakuwa umeshaitazama kazi mpya ya Mbosso ya kuitwa “Amepotea”. Kwa sasa kila kituo cha TV nchini Tanzania bila shaka kitakuwa kinaonesha video hii ambayo imeongozwa na Director Ivan. 

Mbosso kwa takriban miezi 6 sasa alikuwa anatoa video, lakini kati ya zote alizotoa itoshe kusema “Amepotea” ni video bora zaidi kutoka kwake: 

Stori Nzuri 

Video nyingi za sasa za kwenye Bongo Fleva zinazokosa stori kwani mara nyingi wasanii wamejikita lutuonesha set za video na dansi kuliko kuliko kutuhadithia hadithi zitokanazo na nyimbo zao. 

Kwenye “Amepotea” Mbosso anajiachia. Anatupa stori ya mwanaume aliyeondoka nyumbani kwao na kuacha kazi na kwenda kujificha kwa mwanamke huku akipewa mapenzi moto moto. 

Stori ya kwenye “Amepotea” ni ya tofauti na itakufanya uitazame video bila kuchoka kuanzia mwanzo hadi mwisho wa video. 

Ubora Wa Picha 

Video ya “Amepotea” ina ubora wa aina yake na inaweza kuchezwa kwenye kituo chochote duniani kuanzia MTV mpaka Trace bila shaka Director Ivan anatakiwa kupongezwa haswa. 

Rangi ya video bila shaka inavutia ikiwa inaakisi hali ya joto ya jiji la Dar Es Salaam huku hata mitindo ya kuchukulia picha (camera angles) ikiwa inanasa kila kinachoendelea. 

Bila shaka video hii inastahili kuwania kipengelea cha video bora ya mwaka kwenye tuzo za Tanzania Music Awards na nyinginezo nyingi 

Uhalisia Wa Video 

Mbosso amesemea wengi kwenye video yake hii ya “Amepotea” 

Humu ndani Mbosso ameyaanika mandhari ya Uswahilini kwa upana zaidi huku akimulika maeneo ya nyumba za kupanga, masoko na hekaheka zitokanazo na maisha hayo. 

Mwanzoni mwa mwaka huu, Diamond Platnumz alipita njia hii hii kupitia kupitia video yake ya “Yatapita” pamoja na “Zuwena” 

Quick Links

Daily Mixes
DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3
DOWNLOAD LATEST TZ MUSIC MP3
DOWNLOAD LATEST BEST SONGS 2022 MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF TODAY MP3

DOWNLOAD LATEST MUSIC ALBUMS/EP MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF 2023 MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF TODAY MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF THE WEEK MP3

DOWNLOAD LATEST AFRICAN MUSIC MP3

DOWNLOAD LATEST GHANA MUSIC MP3

DOWNLOAD LATEST KENYA MUSIC MP3

DOWNLOAD MP3 NAIJA MUSIC LATEST

FREE Hot DJ Mixes to Download this Week on Mdundo

Leave your comment