Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Moja ya kitu kinachonogesha kiwanda cha muziki Tanzania ni hulka ya wasanii kupendelea kutoa ngoma mya mara kwa mara na ndio maana tumekuandalia orodha ya nyimbo mpya kali kutoka Tanzania ambazo zimetetemesha kiwanda cha Bongo Fleva wiki hii. 

Kutoka kwa wasanii kama Msodoki Young Killer, Maua Sama, Platform na wengineo, hizo hapa ni ngoma mpya kutoka Tanzania kwa wiki hii : 

Top Playlists: DJ D'Ommy Mixtapes, Luo Ohangla, Bongo HITS, Kalenjin HITS, Khaligraph vs. Nyashinski

Ananipenda - Platform & Marioo 

Platform ameungana na Marioo kukuletea “Ananipenda” ngoma kali ya Bongo Fleva ambayo ndani yake Platform na Marioo wanajigamba na kusifia namna ambavyo wanapendwa na wapenzi wao. 

Yamenizidi - Maua Sama 

Wakati mashabiki wanaendelea kusubiri albamu yake ya “Love Waves” Maua Sama ameamua kuwaonjesha wapenzi wa muziki wake ngoma hii mpya ya kuitwa “Yamenizidi”. Humu ndani Maua anachanganya Bongo Fleva na RnB kuonesha jinsi alivyozama penzini. 

Natazama Mbali - Martha Mwaipaja 

Ukisikiliza wimbo huu mpya wa Martha Mwaipaja bila shaka utapata faraja, amani na tumaini la  kuendelea mbele zaidi. “Natazama Mbali” ni wimbo uliopokelewa vyema na wapenzi wa muIki Tanzania 

Born To Win - Msodoki Young Killer Ft Barakah The Prince 

Ili kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Msodoki aliwapa mashabiki zake wimbo huu wa “Born To Win” ambao ndani yake Msodoki anagusia masuala mbalimbali ya maisha ikiwemo wapinzani wake kwenye muziki na mambo mengine mengi sana

I’m Not Fine - Rosa Ree 

Kwenye ngoma yake hii mpya Rosa Ree anazungumza umuhimu wa afya ya akili na mambo mengine mengi kuhusu maisha kwa ujumla. 

Quick Links

Daily Mixes

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

DOWNLOAD LATEST TZ MUSIC MP3

DOWNLOAD LATEST BEST SONGS 2022 MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF TODAY MP3

DOWNLOAD LATEST MUSIC ALBUMS/EP MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF 2023 MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF TODAY MP3

DOWNLOAD LATEST TOP 10 SONGS OF THE WEEK MP3

DOWNLOAD LATEST AFRICAN MUSIC MP3

DOWNLOAD LATEST GHANA MUSIC MP3

DOWNLOAD LATEST KENYA MUSIC MP3

DOWNLOAD MP3 NAIJA MUSIC LATEST

FREE Hot DJ Mixes to Download this Week on Mdundo

 

Leave your comment