Ali Kiba, Ayra Starr Kukutana Jukwaa Moja

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania, Ali Kiba hivi karibuni anatarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa moja na na msanii kutokea huko nchini Nigeria, Ayra Starr.

Ayra Starr ambaye anatoka kwenye lebo ya Mavin ya kwake Don Jazzy anatarajiwa kuja nchini Tanzania na kutumbuiza kwenye tamasha linaloitwa “Reloaded” ambapo msanii huyo atatumbuiza na Ali Kiba. Hii inatarajiwa kuwa mara ya kwanza kwa Ayra Starr kufika nchini Tanzania.

Ayra Starr na Ali Kiba wanatarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa la “Reloaded” Mei mwaka huu ambapo katika tamasha hilo, muigizaji na mwanamuziki Mimi Mars anatarajiwa kuwa mshereheshaji yaani MC

Kando na Ayra Starr, wasanii wengine kutoka Nigeria ambao wameshawahi kufanya tamasha nchini Tanzania ni pamoja na Davido, Wizkid, Burna Boy na wengineo wengi.

Leave your comment