Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii: 'Haratat' Christina Shusho, 'Salama' Rose Muhando Na Wengineo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kiwanda cha muziki nchini Tanzania kimeendelea kupokea bidhaa mpya kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wamepamba wiki hii  kwa nyimbo kali zenye mahadhi ya Amapiano, Bongo Fleva na Muziki Wa Injili.

Kutoka kwa wasanii kama Christina Shusho, Rose Muhando, Rayvanny na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania wiki hii :

Hararat - Christina Shusho

Hatimaye Christina Shusho ameachia album yake ya “Hararat” yenye ngoma 24. Album hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Christina Shusho ndani ya miaka 5 imesheheni collabo kutoka kwa wasanii wa ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Anitha Musoki, Benjamini Weston, Mercy Masika na wengineo wengi

https://www.youtube.com/watch?v=P0k3hFuafJw

Salama - Rose Muhando & Christina Shusho

Malkia wa muziki Tanzania, Rose Muhando na Christina Shusho wameachia wimbo wao wa pamoja wa kuitwa Salama. Wimbo huu umetayarishwa na Abbah Process na ndani yake Christina Shusho na Rose Muhando wanatoa ujumbe uliojaa kutia moyo, tumaini na faraja.

https://www.youtube.com/watch?v=OOF-qCVnstg

 

Gibela Remix - Chino Kid, Rayvanny, S2Kizzy & Mfana Kah Go

Kwenye ngoma hii Chino Kid na Rayvanny wanaungana kwa kusudi la kuwachezesha dansi mashabiki na wapenzi wa muziki wa Amapiano. Utapenda namba ambavyo Rayvanny na Chino Kid wanabadilishana mashahiri mepesi yasiyochosha.

https://www.youtube.com/watch?v=dMxcYfhMfgI

 

Koko - Chino Kidd Ft Loui & Kidlax

Staa anayeendelea kufanya vizuri kwenye Bongo Fleva, Chino Kid ameachia Koko, ngoma kali ambayo ndani yake Chino anatamba kwenye beat la Amapino huku akisaidiwa na Loui ambaye pia ameonesha ufundi mkubwa sana.

https://www.youtube.com/watch?v=Lo0A8Co_U44

 

Ni Wewe - Dr Ipyana

Ni Wewe Ya Dr Ipyana ni wimbo ambao bila shaka utakubariki kutokana na ujumbe na pia itakuburudisha kisawa sawa. Kama unapenda muziki wa Injili basi bila shaka hii ni ngoma maalum kwa ajili yako.

https://www.youtube.com/watch?v=TfRtB3o7JYU

Leave your comment