Christina Shusho Aachia Albamu Ya “Hararat”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kwa takriban miezi minne na zaidi Christina Shusho amekuwa akidokeza kuhusu ujio wa albamu yake mpya na hivi karibuni malkia huyo wa muziki wa Injili nchini hatimaye ameachia albamu yake hiyo mpya ya kuitwa “Hararat”.

Ujio wa albamu ya “Hararat” ulisindikizwa na tamasha kubwa la uzinduzi lililopewa jina la “Mtoko Wa Pasaka” na katika uzinduzi huo, watu mbalimbali mashuhuri kama Diamond Platnumz, Mercy Masika kutokea Kenya, Rose Muhando, Ben Pol na wengineo wengi walipata kuhudhuria.

Albamu ya Hararat imemleta Christina Shusho mpya na ndani ya albamu hii yenye nyimbo 24, Shusho ameshirikisha wasanii tofauti tofauti kutokea Tanzania, Kenya, DRC Congo na Rwanda. Hii ni albamu ya kwanza kutoka kwa Christina Shusho ndani ya miaka 5.

Wasanii wengine wa Injili kutokea Tanzania walioachia miradi ya muziki hivi karibuni ni pamoja na Benjamin Weston pamoja na Gooduck Gozbert ambaye ameachia EP yake ya “Ushindi” hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=AtsA60zvb40

Leave your comment