Kamala Harris Wa Marekani  Ataja Nyimbo Zake Bora Kutoka Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris hivi karibuni ametaja orodha ya nyimbo kutoka Tanzania anazozikubali na kuzisikiliza zaidi.

Kamala ambaye kwa sasa yuko ziarani huko nchini Ghana, ametoa orodha hiyo ambayo imezua gumzo nchini Tanzania ikiwa zimebakia siku chache mpaka Makamu huyo wa Rais afanye ziara yake hapa Tanzania.

Kwenye orodha yake hiyo yenye ngoma 25, wasanii 9 kutoka Tanzania wametajwa. Kutoka WCB Wasafi, wasanii wawili ambao ni Zuchu kupitia ngoma yake ya “Utaniua” pamoja na Mbosso kupitia ngoma yake ya “Shetani” wametajwa katika playlist hiyo ya Kamala Harris.

Ali Kiba pia alitajwa kupitia ngoma yake ya “Mahaba”, Harmonize kupitia “Single Again”, Jux kupitia “Kiss” pamoja na Platform ambapo ngoma yake ya “Fall” aliyofanya na Marioo ilitajwa kwenye orodha hiyo. Ngoma nyingine zilizotajwa ni pamoja na “Lonely” ya Marioo na “Sawa” ya Jay Melody.

Darassa kupitia ngoma yake ya “Nobody” ambayo amemshirikisha Bien alikuwa ndiye rapa pekee kutoka Tanzania aliyeshirikishwa kwenye orodha hiyo ya Kamala Harris.

Leave your comment